|
SOMO LA PILI.
I.
Adhabu za makosa ya
kitabia:
Kumlazimisha mtu kuwa na tabia njema,
hakumfanyi mtu huyo kuwa na tabia njema. Kama ambavyo kumlazimisha mtu
kuamini, hakumfanyi mtu huyo kuwa muumini. Kwani uhuru wa nafsi na
akili, ndio msingi wa majukumu. Na Uislamu unauheshimu na kuuthamini
ukweli huu, nao unajenga fumbulizo la tabia. Ni kwa nini Uislamu utumie
nguvu katika kumjuvya mwanaadamu maana ya kheri, au kumuelekeza
kuiendea? Na ilhali Uislamu una dhana njema na umbile la mwanaadamu na
unaona kuondosha vikwazo vilivyo mbele yake (umbile hilo), kunatosha
kuleta kizazi chenye maadili?
Naam, ni kweli kwamba umbile la mwanaadamu ni jema,
lakini hili halimaanishi kwamba mwanaadamu huyu ni malaika asiye tenda
ila kheri/wema tu. Hapana, bali maana yake ni kwamba huo wema unarandana
na kukubaliana na umbile lake la asili. Na kwamba huo wema kunaathiri
kuukumbatia na kuutenda kwake kama kuruka/kupaa juu kunavyo muathiri
ndege. Hivyo ni pindi pale mwanaadamu huyu anapo jinasua na kamba
(vizuizi) na mizigo (mazito) yake. Kwa hivyo basi, amali sahihi katika
mtazamo wa Uislamu ndio hatua ya mwanzo katika ukataji wa kamba hizo na
ondoshaji wa mizigo. Baada ya hapo, mwanaadamu atakapo lemaa/kita katika
ardhi na asiweze kutukuka, Uislamu humuona mtu huyo kuwa ni mgonjwa,
kisha ndipo humuwepesishia sababu/njia za pozo/shifaa. Na katu Uislamu
hautatoa hukumu ya kumtenganisha mwanaadamu huyu na jamii ila tu pale
kubakia kwake humo kutakuwa kunachochea shari/uovu kwa wengine. Ni ndani
ya wigo wa mipaka hii, ndimo Uislamu unayapiga vita makosa ya kitabia,
kwani mwanzo kabisa Uislamu unawajibisha kwamba mwanaadamu aishi katika
njia tukufu. Na aishi kwa matunda ya mapambano na juhudi yake ya kweli.
Yaani yeye asiujengee uwepo wake juu ya wizi, na ni nini hasa kinacho
mpelekea kuiba? Je, ni kule kuhitajia kwake kile kinacho kidhi
matashi/matamanio yake? Basi hapo na atoshelezwe kwa mahitaji ya lazima,
kiasi cha kumkwasia na kumtoshea na jambo hilo la wizi. Na huo ni wajibu
wa jamii, ukilizembea hilo na hivyo kumpelekea mmoja wao kuiba ili
kutosheleza mahitaji yake. Basi hapo madhambi ya kosa hilo yanaiangukia
jamii iliyo acha kutekeleza wajibu wake na si juu ya yule mwanajamii
aliye tupwa.
Angalia, iwapo jamii itautekeleza wajibu wake huu
kikamilifu, ikamtoshelezea kila mmoja mahitaji yake ya lazima, kisha
baada ya yote hayo akaunyoosha mkono wake kuiba. Hapo kabla ya
kutekelezewa adhabu muafaka, itachunguzwa vema hali yake na huko
kucheleweshwa kwa adhabu ni jambo litakiwalo kidini. Mpaka kufikia Mtume
wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kusema: “Hakika Imamu bila ya
shaka kukosea katika kutoa msamaha, ni bora kwake kuliko kukosea katika
kutoa adhabu”.
Basi itakapo bainika kutokana na kufuatilia hali za mtu
binafsi, kwamba lile umbile lake jema limepondoka/limepogoka na kwamba
yeye amekwisha kuwa chanzo cha uadui kwa mazingira (jamii) yaliyo mlea.
Na kwamba yeye anaipokea huruma na uangalizi wake (hiyo jamii) kwa
kuvunja amani yake na kuchafua usafi wa hali yake. Hapa sasa
mazingira/jamii hii haina lawama, itakapo uhukumu uadui wa mmoja wa
wanajamii, ikaivunja na kuiharibu silaha ambayo anaitumia kuwaudhi na
kuwakera wengine.
Na Qur-ani Tukufu imekwisha ueleza wizi ambao
unastahikisha ukataji wa mkono, ya kwamba huo ni wizi wa dhulma na
uharibifu. Akasema kumuhusu mwizi muadhibiwa huyu: “LAKINI MWENYE
KUTUBIA BAADA YA DHULMA YAKE, NA AKATENGENEA, BASI ALLAH ATAPOKEA TOBA
YAKE. HAKIKA ALLAH NI MWENYE MAGHFIRA NA MWENYE KUREHEMU”. [05:39]
Utaona kupitia aya hii kwamba adhabu iliyo wekwa na Uislamu, hiyo ni
hifadhi ya jamii adilifu tengenefu, dhidi ya madhara/uadui wa mmoja wa
wanajamii. Anaye ukabili uadilifu wa jamii yake kwa dhulma na anaupokea
utengenefu/wema wake kwa ufisadi/uharibifu.
Huo ni mfano tunao uleta ili kubainisha chini ya kivuli
chake kwamba adhabu zitolewazo juu ya makosa ya kitabia. Hazikuwekwa ili
kulazimisha maadili mema na kuwashurutisha watu kwa njia ya nguvu,
kufuata maadili mema. Kwani njia ya kupigiwa mfano iliyo nayo Uislamu,
ni kusema na moyo wa mwanaadamu. Na kuzichochea shauku zake zilizo
jificha kuelekea kwenye utukufu (utu) na ukamilifu na kumrejesha kwa
Allah Muumba wake Mtukuka kwa muundo/njia ifaayo; yaani kwa kukinaisha
na mahaba.
Na ni wajibu kuzitawala hali za mazingira yanayo
mzunguka mwanaadamu ili zisaidie kuivisha vipaji vema. Na wala si makosa
kuving’oa vimelea visivyo na faida, kwani sisi tuko katika makonde
tofauti tofauti ya kilimo. Tunahakikisha ukuaji wa mazao makuu, kwa
kung’oa majani na magugu mengi. Kama hivi ndivyo ulivyo umuhimu wa
kulinda maslahi ya watu wote. Kwa adhabu za makosa ya jinai zilizo wekwa
na kukubaliwa na Uislamu. Adhabu ambazo zimetangulia kutajwa na Taurati
na zikazingatiwa kuwa sharia za dini zote za mbinguni.
Uislamu unaibebesha jamii sehemu kubwa ya jukumu la
kuelekeza kheri au shari na kueneza maadili mabaya au mema. Na Uislamu
kuelekea kwake kutawala nafasi za hukumu, ni kwa sababu ya kutaka kuunda
jamii kwa mfumo utakao saidia kujizuia na maovu na machafu na kuwa
katika mstari nyoofu.
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amepokea kisa
cha muuaji aliye taka kutubia madhambi yake na kwamba yeye “Aliuliza
mjuzi wa watu wa ardhini, akafahamishwa kwa mwanachuoni mmoja.
Akamwambia: Ya kwamba yeye ameua watu mia, basi je anayo toba?
Mwanachuoni yule akamwambia: Nenda kwenye nchi kadha, kwani huko kuna
watu wanao muabudu Allah, basi nawe muabudu Allah pamoja nao. Na wala
usirejee kwenye nchi yako, kwani hiyo ni nchi ya uovu”.
Bukhaariy-Allah amrehemu.
|