SOMO LA
KWANZA
KUIPENDA NCHI (UZALENDO)
Uzalendo, mtu kuipenda nchi
yake ni miongoni mwa tabia njema
ambazo inatakiwa ziwe ni pambo la Muislam.
Tabia hii ina athari kubwa sana katika kuchochea maendeleo ya mtu
binafsi na nchi yake kwa ujumla. Uzalendo
humsukuma mtu kuithamini na kuionea fakhri nchi yake, vitu ambavyo ni
chachu na hamira ya maendeleo.
Uzalendo humfanya mtu kuitakia mema nchi yake kama tunavyosoma
ndani ya Qu-ani: (
Na kumbukeni khabari hii nayo); ALIPOSEMA
IBRAHIMU ; EE MOLA
WANGU! UFANYE MJI HUU (wa Makkah) UWE WA
SALAMA NA UWAPE WAKAZI WAKE MATUNDA ……(2:126)
Hii ni darsa ya uzalendo
ndani ya Qur-ani Tukufu, huku ndiko kuipenda nchi tunakokusudia. Nabii
Ibrahim Amani imshukie ni mfano na kigezo cha uzalendo halisi
mwenye kuipenda nchi yake. Ushahidi
wa hilo ni kule kuiombea kwake nchi yake iwe ni nchi ya amani.
Kwa nini basi Nabii Ibrahim asiombee nchi yake utajiri
au kitu kingine kisichokuwa amani ?
Hili ni kutokana na kuyakinisha kwake kuwa utajiri pasipo amani
haina thamani (maana). Ni chini ya anga la amani tu ndipo wananchi wa nchi
yeyote ile huweza kufaidika na neema zilizomo katika nchi yao na wakapiga
hatua ya maendeleo. Ni chini
ya anga la amani na utulivu ndio huweza kuwa na makini ya kumuabudu
Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hapa
ndipo unapojitokeza umuhimu wa sifa/tabia hii ya uzalendo katika uma/jamii
ya wanadamu. Hebu tuzidi
kuipa nafasi Qur-ani Tukufu izidi kutuonyesha uzalendo wa Nabii Ibrahim,
tusome na tuwaidhike; MOLA
WETU ! HAKIKA MIMI NIMEWAWEKA (nimewakalisha)
BAADHI YA KIZAZI CHANGU (Mwanangu Ismail na mama yake Hajara)
KATIKA BONDE (hili la Makkah) LISILOKUWA NA MIMEA YEYOTO;
KATIKA NYUMBA YAKO TAKATIFU (ya Al-Kaaba) MOLA WETU WAJAALIE
WASIMAMISHE SWALA. NA UJAALIE
NYOYO ZA WATU ZIELEKEE KWAO (wapende kuja kukaa hapa ili pawe mji)
NA UWARUZUKU MATUNDA ILI WAPATE
KUSHUKURU (“ 14: 37).
Tunasema uzalendo ni
mtu kupenda nchi yake hebu tujiulize nchi ni nini kwa sababu ni muhali
kukipenda usichokijua na ndio maana tukawa na msemo usemao “ ASIYEKUJUA
HAKUTHAMINI” Tunaweza
kuelezea nchi kuwa ni pale mahala ambapo mtu amezaliwa katika ardhi yake
na kukulia chini ya anga lake, akifunikwa nalo na kuvuta hewa yake na
kulishwa na mimea ya ardhi yake na kunywa maji yake.
Hii ndio nchi tunayokusudia mtu awe na uzalendo nayo.
Naam, uzalendo ni
kupenda nchi yako sasa kuipenda nchi ndio kufanyaje?
Mtu afanyeje ndipo aambiwe/aonekane kuwa ni mzalendo wa nchi yake?
Kuipenda nchi ni kufanya kila jambo ambalo kwa namna moja au nyingine
litakuwa ni sababu ya kuletea maendeleo, heshima, kuilinda dhidi ya maadui
zake, kuhifadhi, rasilimali (mali asili) zake kwa faida ya kizazi hiki
kilichopo na kijacho. Kujenga
nchi katika msingi ya usawa, haki za binadamu na msingi ya ucha Mungu,
watu wamtambue, wajue na kisha kumuabudu Mwenezi Mungu aliyewaumbia nchi
yao na vyote vilivyomo humo. Hilo
ndilo agizo la Mwenyezi Mungu Mtukufu wa Makureshi bali kwa watu wote kwa
sababu Qur-ani ni mwongozo kwa watu wote:
BASI NA WAMUABUDU BWANA WA NYUMBA HII (AL-KAABA)
AMBAYE ANAWALISHA (wakati Waarabu wenziwao wamo) KATIKA NJAA NA
ANAWAPA AMANI (wakati wenziwao wamo) KATIKA KHOFU (102: 3 – 4).
Ni muhali bali uongo
mweupe mtu kudai kuwa anaipenda nchi yake huku anasahau kumuabudu na
kumshukuru yule aliyemuumbia nchi hiyo na kujazia humo neema zake.
Kilelezo na nembo kuu ya kuonyesha taswira ya uzalendo wa mja kwa nchi
yake kiwe ni kumshukuru Mola Muumba wake na Muumba wa mbingu na ardhi
ambamo humo ndimo nchi yake imo; Shukrani
za kweli ni zile ziambatanazo na ibada ambayo nayo inaangukia katika
matapo/mapote mawili makuu; maamrisho
na makatazo. Hii ni sawa na
kusema ibada ni kutenda tu liloamrishwa na Mola wako na kuacha kutenda
ulilokatazwa na Mola wako. Tunatarajia
kutokana na maelezo yetu hayo kuwa kumbe kuipenda nchi yako ni katika
jumla ya ibada na ni sehemu miongoni mwa sehemu zinazoiunda dini.
Ni wajibu na jukumu la kila mmoja wetu kuipenda nchi yake. Mwanafunzi mwenye uzalendo na nchi yake ni yule anayesoma kwa
hima juhudi na bidii huku akizingatia
miiko na taratibu za elimu ambazo ni pamoja na kwaheshimu waalimu
wake na kanuni zote za shule sambamba
na kushirikiana na wenzake. Mwanafunzi
mzalendo huyu huyafanya yote haya kwa lengo la kupata stadi, maarifa, na
ujuzi ili aweze kuitumikia nchi yake.
Mfanya biashara mpenda nchi yalke ni yule aliye muaminifu katika
biashara yake, hafanyi udanganyifu katika biashara yake kwa kuwauzia
wananchi wenzake bidhaa zilizo chini ya kiwango cha ubora, hawapunji
katika mizani, hawauzii kwa bei ya juu kupita kiasi.
Huitoa haki ya Mungu Mnemeshaji wake (Zakah) kuwapa wananchi
wenzake wenye hali duni. Mfanyakazi
Mzalendo ni yule afikaye kazini mapema kwa muda utakiwao na kufanya kazi
kikamilifu kwa mujibu wa taratibu za kazi,
Ni yule atokaye kazini kwenda nyumbani
kwa muda uliopangwa . Ni
yule asiyedai rushwa kwa kuteekeleza wajibu wake.
Ni yule mwenye mashirikiano mema na wafanyakazi wenziwe hata wale
walio chini yake kikazi. Kauli
ya jumla, mzalendo halisi ni yule ayatangulizae maslahi ya nchi yake mbele
ya maslahi yake binafsi. Ni
yule anayeshirikiana na wananchi wenzake katika kuijenga na kuendelkeza
nchi yao kwa kuifanyia kazi kauli tukufu ya Mola wake
Mtukufu.“…………….NASAIDIANENI
KATI KA WEMA NA TAQWA” WALA
MSUSASAIDIANNE KATIKA DHAMBI NA UADUI” (5:2). Hakuna
hata mmoja anayeweza kuthubutu kusema kuwa kushirikiana katika
kuijenga nchi si katika mema na Taqwa, ikiwa yupo
basi Qur-ani inasema “…………………HAYO NI KWA SABABU WAO
NI WATU WASIO NA AKILI” (5: 58)
Rejea historia
umuangalie mzalendo mkweli mwenye uchungu na nchi yake, Bwana Mtume
Rehema na Amani zimshukie – namna alivyoshirikiana na Makurayshi
wenziwe, waumini na makafiri wao katika kujenga nchi yao ya Hijaazi
(Makkah) yakutoshe kuuona uzalendo na Mtume kwa nchi yake maneno yake
aliyoyasema wakati anatoka Makkah kwenda madinah akiwakimbia jamaa zake
waliokula njama kumuua kwa sababu tu ya Uislamu aliowaletea Mtume
alipompanda ngamia wake tayari kwa safari ya Madinah, aliutazama mji wa
Makkah kwa kitambo kwa macho ya kuuaga kisha kasema
“ WALLAH “ HAKIKA wewe
(Makkah) ndio ardhi ya Mwnyezi Mungu iliyo kipenzi mno kwangu (nipendavyo
zaidi kuliko zote hata huko Madinnah niendako)
Nawe ndiwe ardhi ya Mwenyezi Mungu aipendayo kuliko zote.
Lau si kwa sababu ya watu wako (Makurayshi) kunitoa (kunifukuza)
ndani yako kwa nguvu (kwa hukata kuniua kwao) basi msingelitoka
(ninsingehamia Madinah).
Naam, wamesma kweli
waliosema Mtu kwao. Ukishindwa kuiona picha ya uzalendo wa Mtume kupitia
meneno yako haya, itakuwa ni moja kati ya mambo mawili ima hutaki tu au
akili yako haiakilishi (haifanyi kazi iliyoambiwa ) sasa kama huo
si uzalendo na kuupenda nchi ni nini basi tuambie.