|
3.
Kutenda kitendo kilichokatazwa
kwa
kusahau,
ikiwa
makusudi
yake
hubatilisha
swala. Mithili
ya mwenye kuswali kuzungumza maneno
machache au kuongeza rakaa moja kwa
kusahau. Kisha akazinduka na kutambua
kuwa yumo ndani ya swala, huyu katika mazingira
haya ataleta
sijida mbili za kusahau.
4.Kugurisha/kuhamisha
kitu miongoni mwa
matendo ya swala kukipeleka mahala si
pake. Kikiwa kitu hicho ni nguzo/faradhi
au ni
suna ya “Ba’adh”.
Mfano wa haya ni mtu kusoma
Suuratil–Faatihah (Al-hamdu) katika
kikao (mkao) cha Tashahudi badala
ya mahala
pake ambapo ni katika Qiyaamu (kisimamo
cha
swala). Au mtu kusoma Qunuut katika
rukuu badala ya mahala
pake ambapo ni
katika
Itidali ambayo huja baada ya kurukuu.
Au mtu kuisoma
sura ambayo ni suna, kuisoma
baada ya Al-hamdu katika Itidali badala
ya mahala
pake ambapo
ni katika Quyaamu. Ni suna kwa mtu huyu kusujudu sijida mbili za
kusahau mwishoni mwa swala yake
kutokana
na kuyafanya haya.
vii/.
NAMNA YA
KUSUJUDU SIJIDA ZA KUSAHAU
NA MAHALA PA KUSUJUDU:
Kusujudu kwa kusahau
ni sijida mbili kama
sijida nyingine za swala. Mwenye
kuswali atanuia kwa sijida mbili hizo
kusujudu kwa
kusahau. Na mahala pa kusujudu ni
mwishoni mwa
swala yake
kabla ya
kutoa
salamu. Angalia lau mwenye kuswali atatoa
salamu kabla ya
kusujudu kwa
makusudi
au kwa
kusahau na muda (kitambo) ukarepa
(ukarefuka), itafutu sijida
hiyo. Kama
utakuwa
haukupita muda mrefu, itamuelea
kuidiriki
sijida
ya kusahau kwa kusujudu
mara mbili kwa nia ile ile ya kusahau,
kisha atoe salamu kwa mara nyingine tena.
TANBIHI:
1.Kama mwenye kuswali
hakuleta sijida ya
kusahau ambayo hukumu yake
ni suna, swala yake haitabatilika. Hii ni kwa sababu sijida ya
kusahau haikuwekwa
kwa ajili ya kuacha tendo la wajibu.
2.
Ama mwenye
kuswali atapoacha mojawapo ya
nguzo
za swala
kama rukuu au kusoma
Al-hamdu. Basi hana budi
kuileta nguzo hiyo aliyoiacha wala
kusujudu kwa kusahau
hakutakuwa kiungo cha
nguzo hiyo. Bali sijida mbili za kusahau zitakuja baada ya kuileta hiyo
nguzo
aliyoisahau.
KIAMBATISHI
SIJIDA
ZA MSOMO.
Ni
suna thabiti kutoka kwa Bwana
Mtume–Rehema na Amani
zimshukie–kusujudu
sijida ya msomo. Suna hii inawahusu wote
wawili; msomaji wa Qur-ani na
msikilizaji, iwe ni ndani ya
swala au nje ya swala.
I/.
SABABU YA KUSUJUDU SIJIDA YA MSOMO:
Suna ya sijida ya msomo inapatikana
kwa moja
ya mambo mawili haya:-
1.Kusoma
aya ya Qur-ani ambayo ndani yake
kuna paliposuniwa kusujudu, au
2.Kuisikia
aya hiyo ikisomwa na mtu mwingine.
II/.
DALILI/USHAHIDI
WA SIJIDA YA MSOMO:
Kama tulivyokwishaeleza kwamba
sijida ya msomo ni suna iliyothibiti
kutoka kwa
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Na
ushahidi ni hadithi zifuatazo:-
-
Imepokelewa
kutoka kwa Ibn Umar–Allah awawiye radhi–
amesema: Alikuwa Mtume wa Allah–Rehema
na Amani zimshukie –akitusomea sura
ambayo ndani yake kuna sijida. Basi
(hapo) husujudu nasi husujudu (pamoja
nae) kiasi
hata mmoja wetu hapati mahala pa
kuliweka paji lake la uso (kutokana na
wingi wa watu)”.
-
Na
katika riwaya iliyopokelewa na Abuu
Daawoud: “Mtume– Rehema
na Amani
zimshukie-alikuwa akitusomea Qur-ani.
Anapoipitia (aya ya) sijida
hukabiri na
kusujudu, nasi tukasujudu pamoja nae”.
III/.
FADHILA ZA SIJIDA YA MSOMO:
Imepokelewa kutoka kwa Abuu
Hurayrah-Allah amuwiye radhi-kutoka kwa Mtume wa
Allah-Rehema
na Amani zimshukie–amesema:
“Mwanadamu ataposoma aya ya sijida na
akasujudu, shetani hujitenga na kulia
akisema: Ee
ole wangu, mwanadamu ameamrishwa
kusujudu
akasujudu, basi yamuelea kupata
pepo ya
Allah.Nami
nimeamrishwa kusujudu
nikakhalifu amri ya (Mola
wangu ), basi nitaingia motoni”. Muslimu.
IV/.
HUKUMU YA
SIJIDA YA MSOMO:
Sijida ya msomo hukumu yake ni
suna ambapo mtu akisujudu hupata thawabu
na akiacha kusujudu hapati dhambi. Lakini
tu atakuwa amejidhulumu mwenyewe fursa
ya kujaza na kuithakilisha
mizani yake ya kheri. Dalili ya
haya ni hadithi zifuatazo:-
-
Imepokelewa
na Sayyidna Umar–Allah
amuwiye
radhi–amesema Mtume wa
Allah–Rehema na
Amani zimshukie: “Enyi watu hakika
sisi (tunaposoma Qur-ani) tunazipitia aya
za sijida. Atakayesujudu (mahala
hapo) hakika atakuwa
amesibu (amepatia )
na asiyesujudu, basi hapana
dhambi juu yake”.
Bukhaariy
-
Na
imekuja katika riwaya ya Ibn
Umar–Allah awawiye
radhi:
“Hakika hakutufaradhishia
kusujudu ila tutakapo”.
V/.
SHARTI ZA SIJIDA
YA MSOMO:
Sharti zilizoshurutizwa katika sijida ya
msomo ni nafsi ya sharti
zilizoshurutiziwa swala. Sharti hizo
ni pamoja
na
Na
baki ya sharti nyingine zilizotajwa katika
kusihi kwa swala.
VI/.
NAMNA YA
KUSUJUDU SIJIDA YA MSOMO.
Ni kusujudu
msomaji na msikilizaji wa Qur-ani
anapoifia
aya
ya sijida.
Kusujudu sijida moja iliyo baina ya takbira
mbili, takbira
ya kuliweka paji la uso juu ya
ardhi
na takbira
ya kuliinua
kutoka hapo. Kisha
hutoa salamu na wala hasomi Tashahudi.
Imependelewa kwa mtu mwenye kusujudu
sijida ya
msomo amuombe Allah kwa dua njema, hii
ni kwa sababu katika sijida ndipo mahala
mja huwa karibu zaidi na Mola
wake. Kwa mantiki hii na kujibiwa dua
akiomba pia huwa karibu zaidi mahala hapo
kuliko mahala pengine.
VII/.
MAHALA ZILIMO SIJIDA ZA MSOMO:
Jumla ya sijida za msomo ndani ya Qur-ani
Tukufu ni kumi na tano kama ifuatavyo:-
SURA
AYA
-
Al-a’araaf
(7)
:206
-
Ar–ra’ad
(13)
:15
-
An-nahl
(16)
:49
-
Bani
Israil
(17)
:107
-
Maryam
(19)
:58
-
Al–Hajj
(22)
:18
-
Al–Hajj
(22)
:77
-
Al–Furqaan
(25)
:60
-
An–naml
(27)
:25
-
As-sajdah
(32)
:15
-
Swaad
(38)
:24
-
Fuswilat
(41)
:37
(Ha-Miym–sajdah)
-
An–najm
(53)
:62
-
Al-inshqaaq
(84)
:02
-
Al-alaq
(96)
:19
|