Last Update :  15 Julai 2010 (Alkhamisi)
   3 Shaabani  1431 AH

Makala
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu  
Uliza Suala la dini
Jiunge  !!!
 
 
  Karibu kwenye Mtandao wa UISLAMU  

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5


Dondoo za wiki

Liani
Ujuvyo/fasiri ya liani:
         Neno “liani” kilugha lina maana ya “kufukuza” na “kutenga/kuweka mbali”, kutokana na maana hii tunapata ibara: ALLAH AMEMLAANI – yaani amemfukuza na kumtenga.
Na “liani” imeitwa hivi kwa sababu ya kila mmoja wa wanandoa kuwa mbali na mwenzi wake.
Ama “liani” katika sheria: Ni maneno maalumu yaliyo wekwa kuwa hoja kwa aliye songeka kumtuhumu machafu yule aliye kiboronga uchafu kitanda chake na akampatia aibu.Na imeitwa “liani”, kwa kuwa maneno hayo yamekusanya tamko la laana na kwa kuwa kila mmoja wa wanao laaniana anajitenga na mwenzake kwa sababu ya hiyo liani.
Endelea ....


Moyo kusalimika na mafundo  
Hakuna kitu kinacho mpa mtu raha mno, wala hakuna kitu kinacho muondoshea kabisa mtu jakamoyo, wala hakuna kitu kinacho lituza mno jicho la mtu, kuliko mtu huyo kuishi hali ya kuwa salama wa moyo. Akiwa ametakasika na kihoro cha chuki na mchemko wa mifundo/madonge. Anapo iona neema inamuendea mtu yeyote, huridhia na akazihisi fadhila za Allah katika neema hiyo na uhitaji wa waja wake kwa neema hiyo. Na si hivyo tu, bali akaenda mbali zaidi hata akaikumbuka kauli ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-isemayo: “Ewe Mola wa haki! Neema yoyote iliyo nipambazukia au iliyo mpambazukia yeyote katika viumbe wako, basi hiyo inatoka kwako peke yako na wala huna mshirika. Basi himidi (sifa njema) zote na shukrani zote ni zako wewe”. Abu Daawoud-Allah amrehemu. 
Endelea .....


Ufunguzi wa mji wa Shamu
Tukirejea nyuma, tuliwaacha Waislamu huko Yarmouk wakiwa washindi, walio nusurika baada ya mapambano makubwa. Na amiri jeshi akiwa ni yule muaminifu wa uma huu; Abu Ubeidah Aamir Bin  Al-Jarraah Al-Aamiriy Al-Qurashiy (Mkuraishi wa ukoo wa Aamir), aliye shika uamiri baada ya kamanda panga la Allah; Khalid Bin      Al-Waleed Al-Makhzumiy Al-Qurashiy (Mkuraishi wa ukoo wa Makhzuum). Na wakati huo ilimfikia amiri jeshi habari ya kwamba Warumi walio timshwa mbio wameenda Fihli; eneo katika nchi ya Shamu palipo tokea mapambano baina ya Waislamu na Warumi. Na kwamba msaada mkubwa wa jeshi na zana umekuja Damascus kutoka kwa mfalme wa Urumi. Hapo ndipo amiri jeshi; Abu Ubeidah alipo muandikia waraka Sayyidna Umar akimtaka ushauri, aanze na upi kati ya miji miwili ile?  Endelea ...


Mazungumzo juu ya upweke wa Allah ...Inaendelea
TATU: Katika jumla ya njia za ukinaishi wa hoja ambazo zimefuatwa na Qur-ani Tukufu katika kuwalingania watu kuelekea katika kumtakasia ibada Mola Muumba wao. Ni kwamba imezielezea kwa uaminifu na umaudhui zile shubuhaati (mikanganyo) ambazo washirikina wanazitolea hoja katika kumuabudu kwao asiye Allah. Kisha ukazirudi kwa hoja zinazo ziondosha na kuuweka wazi ubatili wake. Endelea ...

 

Nyakati za Swala
Tafsiri ya Qur-an

Aya ya Wiki

“ENYI WATU! HAKIKA SISI TUMEKUUMBENI KUTOKANA NA MWANAMUME NA MWANAMKE. NA TUMEKUJAALIENI KUWA NI MATAIFA NA MAKABILA ILI MJUANE. HAKIKA ALIYE MTUKUFU ZAIDI KATI YENU KWA ALLAH NI HUYO ALIYE MCHAMNGU ZAIDI KATIKA NYINYI. HAKIKA ALLAH NI MWENYE KUJUA, MWENYE KHABARI”. [49:13]

 

Hadith ya Wiki

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Uadilifu ni jambo jema (kwa kila kitu), lakini kwa viongozi ni jambo jema mno. Ukarimu ni jambo jema, lakini kwa matajiri ni jambo jema mno. Uchamngu ni jambo jema, lakini kwa maulamaa ni jambo jema mno. Subira ni jambo jema, lakini kwa mafakiri ni jambo jema mno. Toba ni jambo jema, lakini kwa vijana ni jambo jema mno. Haya (aibu) ni jambo jema, lakini kwa wanawake ni jambo jema mno”. Dailamiy-Allah amrehemu.

 

Katazo la Wiki

Sote tuna haki katika ardhi hii iliyo umbwa na Allah kwa ajili yetu, ni kweli. Kupitia utaratibu wa kanuni tulizo jipangia wenyewe mtu anamiliki kipande cha ardhi hii ya Allah kwa ajili ya maskani, kilimo na kadhalika. Unajua kabisa kwamba eneo hili ni milki ya fulani, kwa kuwa unaitaka wewe unaunda mizengwe na kwa msaada wa pesa zako unamdhulumu, kwa nini lakini?! Acha, kwani dhuluma hiyo haitakuletea ila ghadhabu za Allah mmiliki wa kweli wa ardhi: “Atakaye jikatia (kipande cha) ardhi ilhali anadhulumu, huyo atakutana na Allah (siku ya Kiyama) hali ya kumghadhibikia”. Ibn Maajah-Allah amrehemu.

 

Swali la Wiki

SWALI: Riba tunayo pewa kwa kuweka pesa zetu katika mabenki ya riba, hatuitumii kwa kuwa ni haramu. Je, tuendelee kuyaachia mabenki hayo au tuichukue na kuitumia katika maslahi ya Waislamu?

JIBU: Katika mas-ala haya, wanachuoni wetu-Allah awarehemu-wamesema: Mwenye kuwa na mali ya haramu, ni wajibu ajitakase nayo kwa namna/sura ambayo hatonufaika nayo yeye binafsi. La si katika kujivutia maslahi yeye, kama vile kutumia katika kula, kunywa, maskani, matumizi ya familia, karo ya shule na kadhalika. Na wala sio katika kujiondoshea madhara au dhuluma, kama vile kutumia katika gharama za bima ya lazima au baki ya aina nyingine za kodi na ushuru. Na wakati wa kuitoa mali haramu hiyo, nia iwe ni kujitakasa nayo na sio sadaka, kwa sababu Allah ni Mzuri hakipokei ila kilicho kizuri (cha halali).

Ama uringo ambamo hutumiwa humo mali za riba, huwa ni katika njia mbali mbali za kheri, mfano: Kuwapa mafakiri na masikini, gharama za matibabu kwa wahitaji, wenye madeni, harakati za vituo vya Kiislamu na kama haya.

Mali haramu, huwa ni haramu kwa mchumaji wake. Ama kwa mwenye kupewa, kunamjuzia kufaidika nayo na kwake huzingatiwa kama mali iliyo potea, isiyo na mwenyewe.

Allah ndiye Mjuzi mno.


| Tuandikie |

: