KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

DONDOO ZA WIKI

UISLAMU NA MASUALA YA UZAZI-LENGO KUU LA NDOA NI KUPATA WATOTO

Uhai hautaendelea au kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba wanadamu hawataendelea kuwepo katika ulimwengu huu kama hakutakuwepo kuzaliana. Huku kuzaliana ndiko kutadhamini mfuatano wa kizazi (generation) baada ya kizazi Wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu alipompa mwanadamu dhima ya kuwa Khalifa ulimwenguni hapa.

Endelea

ADABU ZA DHIFA (TARATIBU ZA KUMPOKEA MGENI NA KUMKARIBISHA MGENI)

Muislamu Mkamilifu wa Imani anaamini uwajibu wa kumkirimu mgeni wake na kumpa heshima na taadhima anayostahiki kwa mujibu wa sheria.

Haya yote ni natija ya kuifanyia kazi kauli ya Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshukie - :

 "Yeyote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho, basi na amkirimu mgeni wake" Bukhariy na Muslim.

Endelea

SAFARI YA PILI YA SHAMU

Bi Khadijah binti Khuwaylid, Bibi mkureshi alikuwa ni mwanamke mwenye tabia njema, anayekubalika na kuheshimika katika jamii ya watu wa Makkah.

Mbali na sifa hizi, Bibi huyu alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa wa mji wa Makkah, alipenda sana kufanya biashara.

Kutokana na kuona mbali na upevu wa akili yake alikuwa akiizalisha mali yake kwa kuwaajiri watu. Aliwapa mali wakaiuze kwa mkataba na kuwapa sehemu ya faida iliyopatikana.

Habari za tabia murua, uaminifu na ukweli wa Bwana Mtume – Rehma na Amani zimshukie – zilipoyagonga masikio ya Bi Khadija; akajawa na raghba ya kutaka kumuhusisha mtu huyu mwaminifu na mkweli katika biashara yake.

Endelea

UDHU NA NAMNA YA KUTAWADHA

i) MAANA YA UDHU :

Tamko/Neno udhu linafasirika katika lugha ya kiarabu kama wema, uzuri na ung'avu.

Ama maana ya udhu katika istilahi ya wanazuoni wa fani ya Fiq-hi;

udhu ni twahara inayotumia maji, twahara hii inahusisha viungo maalum vya mwili, baadhi yake hukoshwa kama mikono, uso na miguu na vingine hupakwa maji kama vile kichwa.

Endelea

Additional information