KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

MAJADILIANO NA WATU WA KITABU (MAYAHUDI NA MANASWARA).../Inaendelea/9

Kudai kwao ya kwamba Allah ana mkono wa birika, na Qur-ani ikawajibu kwa majibu rejezi yanayo wafunga vinywa na kuwafanya kubezwa na kudharauliwa na watu wenye akili. Madai na majibu yao yamo ndani ya kauli yake Allah Ataadhamiaye: “NA MAYAHUDI WALISEMA: MKONO WA ALLAH UMEFUMBA. MIKONO YAO NDIO ILIYO FUMBA, NA WAMELAANIWA KWA SABABU YA WALIYO YASEMA. BALI MIKONO YAO I WAZI. HUTOA APENDAVYO. KWA YAKINI YALIYO TEREMSHWA KWAKO KUTOKA KWA MOLA WAKO MLEZI YATAWAZIDISHIA WENGI KATIKA WAO UASI NA KUFURU. NA SISI TUMEWATILIA UADUI NA CHUKI BAINA YAO MPAKA SIKU YA KIYAMA. KILA MARA WANAPO WASHA MOTO WA VITA, ALLAH ANAUZIMA. NA WANAJITAHIDI KULETA UHARIBIFU KATIKA ARDHI. NA ALLAH HAWAPENDI WAHARIBIFU”. [05:64]

 

 

Katika kuelezea sababu za kushuka kwa aya hii, Mufasiruna-Allah awarehemu-wametaja riwaya nyingi. Miongoni mwa hizo ni hii iliyo pokewa kutoka kwa Ibn Abbas-Allah awawiye radhi-ya kwamba mtu mmoja katika Mayahudi aitwaye Shaasi bin Qaysi, alimwambia Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: Ewe Muhammad! Hakika Mola wako ni bakhili, hatoi. Ndipo Allah Ataadhamiaye akaishusha aya hii”. [TAFASIIR IBN KATHIR, Juz. 02, Sah. 74]

 

Allah-utakati wa mawi ni wake-ameitegemeza kauli hii kwa Mayahudi wote, kwa sababu wao hawakumkana msemaji wa maneno hayo na isitoshe wakayaridhia. Na amesema Ikrimah: Hakika si vinginevyo, aliye yasema maneno hayo ni Fanahaaswu bin Aazuuraa na wenzake. Hawa walikuwa na mali mengi, walipo mkufuru Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-mali yao yakapungua, ndipo wakayasema hayo waliyo yasema.

 

Na riwaya nyingine inasema: Kwamba wao walipo muona Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-yumo katika lindi la ufakiri na uchache wa mali na wakaisikia kauli yake Allah Ataadhamiaye: “NI NANI ATAKAYE MKOPESHA ALLAH MKOPO MWEMA...”, wakasema: Hakika Mungu wa Muhammad ni bakhili.

 

Na kauli yake Allah Ataadhamiaye akiwanukuu: “NA MAYAHUDI WALISEMA: MKONO WA ALLAH UMEFUMBA”. Hiyo ni khabari kutoka kwa Allah ikielezea uthubutu wa Mayahudi juu yake na utovu wao wa adabu kwake. Na ni kuwaumbua kwa ukanushi/upingaji wao wa neema zake zisizo dhibitika.

 

Na walikusudia kwa kusema kwao: “MKONO WA ALLAH UMEFUMBA”: Ya kwamba Yeye Allah-utakati wa mawi ni wake-ni bakhili kwao wao, anazizuia kheri zake zisiwafikie wao, anavifungia vipawa vyake visiwakunjukie. Kama mtu mwenye mkono wa birika, ambaye hawezi kuukunjua kwa kutoa.

 

Na wala hayakuwa mapendeleo ya mkono hapa, kuwa ni kile kiungo cha mwili wa mwanaadamu kijulikanacho kwa jina hilo. Hivyo ni kwa sababu Allah Ataadhamiaye ameepukana na kufanana na vizuka (viumbe). Na hakika si vinginevyo, kufumba na kukunjua mkono ni fumbo mashuhuri linalo elezea unyimi na upaji.

 

Na sababu ya kutajwa mkono, ni kwamba huo mkono ni kiungo kinacho tumiwa katika kutenda matendo mengi, khususan katika utoaji na upaji wa mali. Kwa minajili hiyo basi, ndio msababishaji (mtenda) akapewa jina la sababu, na wakautegemeza ukarimu na ubakhili kwa mkono na kitanga. Hapo ndipo mtu mkarimu akaambiwa: “mfurika wa mkono”, “mkunjufu wa kitanga” na bakhili akaambiwa: “mfumba wa kitanga”. Na ameyaweka wazi maana haya muandishi wa Tafsiri AL-KASSHAAFU, kwa kauli yake: “Kufumba na kukunjuka kwa mkono ni fumbo linalo elezea ubakhili na ukarimu. Na imekuja kwa maana hiyo kauli yake Allah Ataadhamiaye: “WALA USIUFANYE MKONO WAKO KAMA ULIO FUNGWA SHINGONI MWAKO, WALA USIUKUNJUE WOTE KABISA”. Na wala mwenye kuyatamka maneno hayo, hakusudii kuuthubitisha mkono kama kiungo, wala kufunga au kukunjua...”. [TAFSIIR AL-KASSHAAFU, Juz. 01, Sah. 655]

 

Na kauli yake: “MIKONO YAO NDIO ILIYO FUMBA, NA WAMELAANIWA KWA SABABU YA WALIYO YASEMA”. Hii ni dua dhidi yao, uwashukie ubakhili topezi na unyimi mbaya, kwa Allah-utakati wa mawi ni wake-kuwaumbia ubakhili utakao wafanya kutengwa na watu. Na kuondokea hapo ndio Mayahudi wakawa mabakhili mno kuliko watu wote. Na Allah Ataadhamiaye akawahukumia kufukuzwa kwenye rehema za Allah kwa sababu ya utovu wao wa adabu kwake na kwa kuzikanusha kwao neema zake.

 

Na sentensi hii ni mafundisho yatokayo kwa Allah kuja kwetu, ya kwamba tuwaombee dua ya maangamizi wale ambao zimefisidika nyoyo zao na wakamfanyia utovu wa adabu Muumba na Mruzuku wao. Na wakasema katika shani yake yale ambayo Yeye ameepukana nayo: “AMETAKASIKA NA AMETUKA JUU KABISA NA HAYO WANAYO YASEMA”.

 

Na kauli yake: “BALI MIKONO YAKE I WAZI”, maana yake ni: Si hivyo kabisa, enyi Mayahudi! Jambo haliko kama mnavyo dai nyinyi kwa kusema maneno ya batili. Lakini Yeye-utakati wa mawi ni wake-ni Mkunjufu wa fadhila, Mwingi wa vipawa ambaye hapana chochote ila khazina yake iko kwake.

 

Kwa hivyo basi, ukunjufu wa mkono hapa ni fumbo linalo elezea ukarimu, fadhila na uneemeshaji wake kwa viumbe wake.

 

Na tamko la mkono limeletwa kwa muundo wa uwili, akasema: “BALI MIKONO YAKE”, ili kuashiria wingi wa upaji na uneemeshaji. Kwa sababu Mwingi wa upaji na ukarimu anapo taka kutoa sana, hutoa kwa mikono yake yote miwili.

 

Amesema Imamu Ibnu Kathir-Allah amrehemu: Kauli yake: “BALI MIKONO YAKE I WAZI”, yaani: Bali Yeye ni Mkunjufu wa fadhila ambaye hapana neema yoyote waliyo nayo viumbe wake, ila inatoka kwake Yeye pake yake. Kama alivyo sema: “NA MKIHISABU NEEMA ZA ALLAH HAMWEZI KUZIDHIBITI. HAKIKA MWANAADAMU NI DHAALIMU MKUBWA, MWENYE KUZIKUFURU NEEMA”. [14:34]

 

Na aya zinazo lizungumzia suala hilo ni nyingi kathiri.

 

Na amepokea Imamu Ahmad, Bukhaariy na Muslim-Allah awarehemu-kutoka kwa Abu Huraira-Allah amuwiye radhi-amesema: Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Hakika (mkono wa) kulia wa Allah umejaa pomoni, (kilichomo humo) hakipunguzwikutoa, umejaa usiku na mchana. Je, mmekiona alicho kitoa tangu alipo umba mbingu na ardhi, basi hakika hicho hakijapunguza kilichomo (katika mkono wa) kulia wake. Na arshi yake ilikuwa juu ya maji na katika mkono wake mwingine kuna mjao unao inuka na kushuka. Na akasema (Mtume): Toa nikupe”. [TAFSIIR IBN KATHIIR, Juz. 02, Sah. 75]

 

Na kauli yake: “HUTOA APENDAVYO”, hii ni sentensi andilizi, imeletwa kusisitiza ukamilifu wa ukarimu na upaji wake. Na imekuja kudalilisha ya kwamba kwa muktadha wa hekima na matashi yake, Yeye-utakati wa mawi ni wake-humkunjulia riziki amtakaye na humbania amtakaye. Na kumbania kwake riziki amtakaye katika waja wake, hilo halikanushi ukunjufu wa ukarimu wake, kwa sababu Yeye hutoa na huzuia kwa mujibu wa matashi yake ambayo amejengea juu yake utaratibu wa viumbe vyake.

 

Kisha tena Allah-utakati wa mawi ni wake-akabainisha hali yao ya upingaji wa yale aliyo yateremsha kwa Mtume wake, akasema: “KWA YAKINI YALIYO TEREMSHWA KWAKO KUTOKA KWA MOLA WAKO MLEZI YATAWAZIDISHIA WENGI KATIKA WAO UASI NA KUFURU”. Yaani: Ewe Muhammad! Hakika Qur-ani hii Tukufu tuliyo kuteremshia, na mambo yaliyo fichikana ya hao Mayahudi tuliyo kufunulia na hali za wahenga wao. Yote hayo kabisa yatawazidishia wengi wao ukafiri juu ya ukafiri wao, na uasi juu ya uasi wao. Na inakuwa hivyo, kwa sababu wao ni watu ambao nyoyo zao zimeliwa na mifundo/chuki, na hasadi imezitawala nafsi zao.

 

Na yajapo kuwa yale tuliyo kuteremshia wewe, ewe Muhammad! Ndani yake limo ponyo la nafsi za waumini, hakika hayo kwa upande wa hao Mayahudi, yanawazidishia dhuluma na ukafiri. Allah Ataadhamiaye amesema: “NA TUNATEREMSHA KATIKA QUR-ANI YALIYO NI MATIBABU NA REHEMA KWA WAUMINI. WALA HAYAWAZIDISHII MADHAALIMU ILA KHASARA”. [17:82]

 

Kwa hivyo basi, sentensi hiyo tukufu, ni ubainifu wa hali ya upinzani wa Mayahudi, kuzipinga aya alizo ziteremsha Allah kwa Mtume wake-Rehema na Amani zimshukie. Na wakati huo huo, sentensi hiyo ni liwazo kwake Bwana Mtume kutokana na maudhi yanayo mpata kutoka kwao.

 

Na Allah-utakati wa mawi ni wake-ameitilia mkazo sentensi hiyo kwa kiapo, ili kusiwepo kabisa na matarajio ya kuwa iko siku moja Mayahudi watakuwa ni waumini. Na ili Mtume na maswahaba wake waamiliane nao kwa misingi ya yale yaliyo fichwa na nafsi zao mbaya, na nyoyo zao zinazo ugua maradhi ya hasadi na hadaa.

 

Kisha Allah-utakati wa mawi ni wake-akazidi kumliwaza Mtume-Rehema na Amani zimshukie-akawapitishia hukumu yake, ya kudumu uadui na chuki baina ya mapote yao, akasema: “NA SISI TUMEWATILIA UADUI NA CHUKI BAINA YAO MPAKA SIKU YA KIYAMA”.

 

Maana:

 

Na tumetia baina ya mapote mbali mbali ya Mayahudi, uadui wa kudumu na chuki endelevu. Kwa hivyo basi, wewe unawadhania kuwa wako pamoja na ilhali nyoyo zao ziko mbali mbali. Na kila kundi miongoni mwao ni pinzani ya jingine, nao watakuwa katika hali hiyo mpaka siku ya Kiyama.

 

Na kauli yake-utakati wa mawi ni wake: “KILA MARA WANAPO WASHA MOTO WA VITA, ALLAH ANAUZIMA. NA WANAJITAHIDI KULETA UHARIBIFU KATIKA ARDHI. NA ALLAH HAWAPENDI WAHARIBIFU”. Kauli hii ni ubainifu wa kuendelea na kutopea kwao katika maasi na machafu. Na ni bishara kwa waumini walio wakweli, ya kwamba Allah Ataadhamiaye atavirudisha vitimbi vya mafisadi hao, shingoni mwao wenyewe.

 

Yaani: Kila walipo taka kumpiga vita Mtume na waumini na wakaandaa sababu za vita na wakajaribu kuwagawa na kuchochea uadui baina yao. Kila walipo fanya hivyo, Allah aliiharibu mikakati yao, akavipomosha vitimbi vyao na akatia khofu ndani ya nyoyo zao.

 

Na Mayahudi hawa wanafanya jitihada kubwa kuleta maharibiko katika ardhi kwa njia ya kuchochea fitina na kueneza mambo machafu. Na Allah Ataadhamiaye hawapendi mafisadi, bali anawachukia.

 

Kwa maelezo haya basi, tunaiona aya tukufu imekwisha warudi Mayahudi katika kumnasibishia kwao Allah ubakhili. Na imebainisha ya kwamba Yeye-utakati wa mawi ni wake-ni Mkunjufu wa fadhila na ni Mwingi wa upaji. Na ikafichua sehemu ya mabaya yao na upasito wao na ikaweka wazi ya kwamba Yeye-utakati wa mawi ni wake-anawachukia kwa sababu ya kukita shari na ufisadi ndani ya nafsi zao.

 

Additional information