"Mwenyezi Mungu akimtakia kheri Mja humfahamisha (humpa elimu) kwenye dini" Hadith Tukufu

AINA ZA JOSHO, YAWAJIBISHAYO JOSHO NA YALIYO HARAMU KWENYE KUWAJIBISHWA NA JOSHO

Kuna aina mbili za josho kwa mtazamo wa kisheria (kifiq-hi):

  1. Josho la faradhi/wajibu na
  2. Josho la suna
  1. JOSHO LA FARADHI :

Hili ni lile josho ambalo haitosihi ibada yenye kuhitajia twahara kama vile swala bila ya kupatikana kwanza josho hili wakati wa kuwepo sababu zake.

SABABU ZA JOSHO LA FARADHI :

Haya ni yale mambo ambayo yakimtokea muislamu yatamsababishia awajibikiwe kukoga josho hili la faradhi. Mambo hayo ni :

  1. Janaba
  2. Hedhi/Nifasi
  3. Kuzaa/Kujifungua
  4. Mauti (kifo)

Haya ndiyo mambo ambayo humpasia muislamu josho la faradhi yatakapomtokea. Hebu sasa tujaribu kuyafafanua moja baada ya jingine.