"Mwenyezi Mungu akimtakia kheri Mja humfahamisha (humpa elimu) kwenye dini" Hadith Tukufu

MAANA YA TAMKO LA ADHANA

Allaahu Akbar - Allah ni Mkubwa kuliko kila kitu.

Ash-hadu An-laa Ilaaha Illal-laah- Ninashuhudia kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah pekee.

Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah – Ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah.

Hayya Alas-swalaah – Njooni kuswali.

Hayya Alal-falaah – Njooni kwenye kufaulu.

Asswalaa tu khayrun Minan-nawm – Swala ni bora kuliko usingizi.

Allaahu Akbar – Allah ni Mkubwa kuliko kila kitu.

Laa Ilaaha Illal-laah – Hapana aabudiwaye kwa haki ila Allah.

 


(1) Tarji’i ni kuyarudia tena matamko hayo kwa sauti ya chini kidogo.