|
Miongoni
mwa kanuni jumla za uislamu katika vyakula na vinywaji ni Allah
kuwahalalishia waja wake:-
1.
Vilivyo vizuri
2.
Vyenye kuwastarehesha wanapovila au huvinywa
3.
Vyenye manufaa
Na kuwaharamishia vilivyo
vibaya kwa ladha, harufu au madhara. Msingi/kanuni hii inapatikana katika
kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “NA ANAWAHALALISHIA VIZURI NA
KUWA HARAMISHIA VIBAYA” (7:157)
Kwa kanuni hii haijuzu
kisheria kwa mtu yeyote yule kula au kunywa kitu chochote kinachoidhuru
afya yake na kuyatishia (kuyahatarisha) maisha yake. Hii ni kwa sababu
muislamu haimiliki nafsi/roho yake mpaka akawa na uhuru wa kuitumia
atakavyo ikiwa ni pamoja na kutumia yanayopelekea kuingamiza
nafsi/roho hiyo ambayo imo katika milki ya Allah. Uhai wa muislamu
ni haki ya Allah aliyempa uhai huo bila ya maombi, makubaliano wala malipo
yoyote kutoka kwake. Afya ya muislamu ni miongoni mwa neema za Allah
alizomneemesha mja wake huyu, kwa hiyo si halali kwake kuichezea na
kuihatarisha neema hii.
Hakuna
tafauti baina ya mtu mwenye kujiua yeye mwenyewe kwa kitu chenye kuua mara
moja (papo kwa papo) kama kisu, risasi na kadhalika, na yule mwenye kujiua
kwa sumu inayoua taratibu (kidogo kidogo). Wote wawili hawa wanafanya kosa
moja lile lile kwa njia tofauti, huyu anajiua haraka na yule anjiua
taratibu ,wote wana hatiambele ya sheria kwa sababu wanalipinga agizo la
Mola wao:
“…..WALA
MSIJIUE(wala msiue wenzenu) HAKIKA ALLAH NI MWENYE KUKUHURUMIENE”(4:29).
Tuzidi kusoma :
“---
WALA MSIJITIE KWA MIKONO YENU KATIKA MAANGAMIZO---” (2:195)
Tujiulize
ikiwa mtoa uhai anakuhurumia vipi wewe usiyeumiliki uhai huo hujuhurumii
na unajiangamiza wewe mwenyewe, ni akili gani hiyo?!
Ni
vema tukakumbuka pia kwamba mali ni neema ya Allah iliyo juu yetu, kwa
hiyo ni wajibu wetu kuihifadhi na kuitumia vizuri neema hii. Muislamu
hapaswi kuitumia mali ila katika njia/matumizi ya halali tu. Hii ni kwa
sababu Allah ameifanya mali kuwa ndio zana ya maisha ya watu, kwa hivyo
mtu kuifuja mali binafsi ni kuufuja utajiri wa rasilimali ya umma. Kanuni
hii imethibiti katika tamko la Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie
kwamba yeye “Amekataza ufujaji wa mali” Muslim. Kulinda/kuhifadhi maisha (uhai) ya mtu, mali
na akili ndio makusudio na dhima ya sheria ya Kiislamu. Hili
linathibitishwa na adhabu kali zilzozowekwa na sheria dhidi ya mtu
anayechezea au kuhatarisha vitu vitatu hivyo; maisha,mali na akili. Ni
(kupitia katika) chini ya mwangaza wa kanuni na makusudi haya ndio
tunaweza kuuhukumu uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku kwa ujumla
baada ya kujua madhara na athari yake mbaya. Kumbukumbu za kihistoria
zinaonyesha kwamba tumbaku imeanza kutumiwa na wakazi asili wa Amerika,
wahindi wekundu (Red Indian’s) tangu katika karne ya kumi na tano (15th
centuryA.D). Jamii hii ya wahindi wekundu ilitumia tumbaku kwa matumizi
mbalimbali, walitumia kwa kuitafuna,kuitia puani (ugolo) na kwa kuisokota
sigara au kuivuta ndani ya kiko kutoka hapo ndipo ada hii ya uvutaji wa
sigara ikajipenyeza barani ulaya na kuenea pande mbalimbali za dunia.
Baada ya tumbaku kuenea kwa kasi ya moto wa nyikani na kupata wateja wengi
ndipo ilpozidishwa uzalishaji wake na kujengwa viwanda vikubwa. Dhima kuu
ya viwanda hivi ni kuzalisha aina mbalimbali za sigara ili kukidhi
mahitaji za wateja kuanzia hapo uvutaji wa sigara imekuwa ni janga kubwa
kwa jamii ya wanadamu. Umekuwa ni gonjwa hatari la kuambukiza watu
wanapokezana na kuambukizana gonjwa hili. Mdogo anamwiga mkubwa katika
uvutaji, mtoto anamwiga baba yake, maskini anamwiga tajiri, watu wote
wamekuwa ni watumwa wa janga hili wasiloweza kujikomboa nalo.
Ni
baada ya muda mchache tu tangu kuenea kwa matumizi ya tumbaku, madaktari
waligundua matumizi makubwa yanayoipata jamii ya wanadamu kutokana na
utumiaji wa tumbaku katika mwaka 1598 A.D ilitoka kwa mara ya kwanza
nchini Uingereza makala ielezayo madhari na hatari ya utumiaji wa tumbaku.
Kisha zikafuatia tafiti mbalimbali zilizoendelea kugundua na kuelezea
madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku na namna inavyoathiri na
kuhatarisha afya ya binadamu. Matokeo ya tafiti hizi za wanasayansi ya
tiba zilipelekea baadhi ya nchi kama vile Denmark,Uholanzi na Sweden
kuweka (kutunga) sheria zinazozuia
uvataji wa sigara. Lakini baadae serikali hizo zikaona zinapata upungufu
katika bajeti zao kutokana na kukosa kodi kubwa itokanayo na uzalishaji wa
tumbaku na uuzaji wa sigara. Makampuni na mashirika yanayojishughulisha na
uzalishaji na uuzaji wa sigara hutenga fungu kubwa la fedha katika kuitangaza biashara yao
hii hatari.
Madhara
na athari mbaya itokanayo na matumizi ya tumbaku iko wazi sasa kwa kila
mmoja wetu. Sio siri tena kwamba tumbaku ina madhara kwa afya ya binadamu
na ndio maana Shirika la Afya Duniani (WHO)
likayaagiza mashiriki yote yanayozalisha sigara kutangaza kwa
kuandika katika bidhaa zake kuwa "Uvutaji sigara una madhara kwa afya
yako”. Uvutaji sigara unasababisha maradhi mbalimbali kama vile saratani
ya mapafu, wazimu, kupooza matatizo ya mfumo wa hewa (kupumua), kutoboka
kwa utumbo, kunyonyoka nywele, upungufu wa nguvu za kiume, maradhi ya
ngozi na kadhalika. Madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku hayajitokezi
mara moja bali kuchukua miaka kadhaa hata miaka thelathini, ni jambo
ambalo huwafanya watu wengi kufumbia macho madhara hayo ya pole pole na
hivyo kuendelea na tabia ya uvutaji wa sigara. Mvutaji sigara mbali ya
kujidhuru mwenyewe huwadhuru wengine pia kwa kuwalazimisha kuvuta hewa
iliyochafuliwa na moshi wenye sumu ya tumbaku. Mvutaji huwaathiri watu
waliomzunguka, humuathiri mkewe/mumewe, huwaathiri wanawe kama
anavyoyaathiri mazingira aishimo.
UVUTAJI
HUATHIRI AKILI YAKO:
Mwenyezi
Mungu ametuzawadia akili ili itusaidie kufikiri, kutatua na kupanga mambo
yetu mbalimbali. Ni vipi basi mtu mwenyewe akili timamu anathubutu kufikia
uamuzi wa kujidhuru yeye mwenyewe kwa hiyari yake bila kuladhimishwa na
mtu mwingine?! Uvutaji unaiathiri akili yako, kwa sababu ndani ya uvutaji
kuna kiasi fulani cha ulevi unaosababisha ulegevu wa mwili. Hili aneweza
kuliona mvutaji anapovuta sigara kwa mara ya kwanza kabisa. Hawa
wanaotumia mali zao kununua kinachowadhuru
wakati ambapo familia zao zinakosa mahitaji muhimu, nao hawajali.
Hebu tuwe wakweli, watu hawa wana akili kweli?!
UVUTAJI
UNAIDHURU DINI
Kama
ambavyo uvutaji unavyoidhuru akili, na ya maisha mvutaji na watu wengine,
pia huiathiri na kuidhuru dini. Tunawajua baadhi ya watu wasiofunga mwezi
wa Ramadhani. Ukiwauliza kwa nini, hujibu: siwezi kuacha kuvuta sigara,
kwa sababu ndio uhai wangu! Kwa mtu huyu sumu ya sigara inayomuua kidogo
kidogo ni bora zaidi kuliko swaumu inayompa ucha-Mungu na siha njema watu.
Wengi hufunga, muadhini anapoadhini tu
Magharibi futari yao ya mwanzo huwa ni sigara yenye kuwadhuru. Huku ni
kuyapinga na kwenda kinyume na maelekezo na amri ya Bwana Mtume –Rehema
na Amani zimshukie-alipotuambia tufuturu kwa tende, maziwa
au hata maji vitu vyenye faida mwilini. Isitoshe uvutaji sigara
humsukuma mvutaji kufanya ubadhirifu israfu na kuwaudhi wengine, mambo
yote haya yamekatazwa na Allah. Pia ni kweli kuwa mvutaji hawezi kuwa
askari shujaa na mwenye nguvu katika kuipigania dini ya Allah,kuilinda
nchi yake na heshima ya waislamu na uislamu. Kwa nini, hii ni kwa sababu
tayari sumu nya sigara itakuwa imeshamdhoofisha na kuzimaliza nguvu zake.
Je, huku si kuidhuru dini?!
UVUTAJI
WAKO UNAIATHIRI FAMILIA YAKO
Mvutaji
sigara huilazimisha familia yake kuvuta hewa iliyochafuliwa na kutiwa sumu
itokanayo na moshi wa sigara aivutayo na hivyo kumdhuru mkewe, wanawe hata
yule masikini mtoto mchanga anadhuriwa ! Utafiti wa kitaalamu
umedhibitisha kwamba watoto wanaolelewa katika mazingira ya baba/mama
mvutaji huathirika mishipa yao inayosafirisha damu kuipeleka katika moyo.
Hali hii husababisha kuharibika kwa mfumo mzima wa usafirishaji damu
mwilini na kuwafanya watoto hawa wasio na hatia kuwa ni wahanga wa maradhi
mbalimbali. Zaidi ya hayo ni ukweli kuwa mtoto ni kiumbe wa kuiga kizuri
au kibaya, yeye anachojua ni kuiga tu. Kwa mantiki hii, watoto watamuiga baba yao
mvutaji, nao wataanza kuvuta kwa kudhani kuwa huo ndio uanamume na ndio
ustarabu. Janga hili umelileta wewe baba/mama mvutaji, je, huko si
kuidhuru familia yako?! Wewe mama mjamzito mvutaji, elewa kuwa uvutaji
unakudhuru na kumdhuru na kumdhuru mwanao aliye tumboni. Uvutaji wakati
kumdhuru mwanao aliye tumboni. Uvutaji wakati wa ujauzito husababisha:-
1.
Kuathirika kwa suala zima la ukuaji wa mimba kutokana na sumu ya
tumbaku.
2.
Kondo la nyuma {placenta} kushindwa kusafirisha vizuri chakula
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
3.
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito pungufu jambo ambalo litaathiri
ukuaji wake.
4.
Kupungua hamu ya chakula kwa mama mjamzito ambako huchangia kwa
kiasi kikubwa kuathirika kwa afya ya mama na mtoto
Ewe
mama wee! Mbona unamdhulumu na kumdhuru malaika huyu, amekosa nini
masikini huyu?
UVUTAJI
UNAIDHURU MALI (UCHUMI):
Mvutaji
huitumia mali (pesa) yake katika kitu
kisicho na manufaa, si duniani
wala kule akhera. Wanawazuoni wamekongamana kwamba utumiaji wa mali
katika yasiyo na manufaa ni HARAMU haijuzu kabisa kisheria. Ufujaji mali
hauna nafasi kabisa katika Uislamu, Bwana Mtume –Rehema na Amani-
amelikemea na kulikataza hilo. Elewa ewe mvutaji na kila mbadhirifu wa
mali, uliyonayo mali ni mali
ya Allah na wewe ni
mchungaji/mtunzaji wa mali hiyo. Kwa msingi huu huna haki ya kutumia mali
yako katika mambo/vitu visivyo na manufaa kwako. Haviinufaishi roho yako,
mwili wako, akili yako, famalia wala jamii yako. Mvutaji huitumia mali
yake kununua madhara, anajidhuru kwa gharama! Afadhali angekuwa anajidhuru
bure bila ya kutoa gharama hivi hii ndio akili?! Au hii ndio dini?! Au
haya ndio maendeleo na ustaraabu?! Kwa kweli lau si mazoea ya watu kuizoea
tumbaku, mtu asingeliionja, angeliichukia na kuitupilia mbali. Lakina mtu
akizoea kitu hata kama ni kula udongo au mkaa au pilipili kali, basi nguvu
ya mazoea humfanya akione kizuri na kitamu kitu hicho na hili ni janga
jingine! Ewe mvutaji ihurumie nafsi yako, acha leo kuvuta, amua! Ukiwa
unaweza kujizuia kuvuta, masaa kumi na tano (15 hours) ndani ya mwezi wa
Ramadhani unapofunga, kwa nini ushindwe sasa?! Allah anatuambia:-“--- NA
UFUNGAPO NIA MTEGEMEE
ALLAH (tu ili ufanye hili uliloazimia) HAKIKA ALLAH ANAWAPENDA
WAMTEGEMEAO.” (3:159)
Kumbuka
huu ni ushauri nasaha, kunasihika au kutonasihika au kutonasihika hilo ni
shauri lako
|