|
TUJIULIZE:
1·NINI
MTIZAMO WA UISLAMU KATIKA
SUALA LA HIJABU KWA MWANAMKE
NA HAKI YAKE YA KUSOMA NA KUFANYA KAZI.
2·JE
NI KWELI KUWA HIJABU HAIENDI SAMBAMBA NA MAISHA YA LEO? (IMEPITWA NA
WAKATI).
Kwanza
kabisa ni vema tukaelewa tunapozungumzia
Hijabu tunazungumzia nini. Tunapoizungumzia Hijabu tunaikusuduia Hijabu
kama ilivyo ndani ya Qur - ani Tukufu. Neno Hijabu limetumika ndani ya Qur
- ani zaidi ya mara nane. Miongoni mwa aya zilizoitaja Hijabu ndani ya Qur
- ani ni hizi zifuatazo:-
"..
NANYI MNAPOWAULIZA (wakeze Mtume) WAULIZENI NYUMA YA PAZIA (Hijabu) ..." (33:53)
Hii
ndio Hijaabu kwa lugha ya Qur - ani:-
"(NA
WAKASEMA: "NYOYO ZETU ZI KATIKA VIFUNIKO KWA YALE UNAYOTUITIA; NA
KATIKA MASIKIO YETU MUNA UZITO; NA BAINA YETU NA BAINA YAKO KUNA
PAZIA. (Hijaabu) ???" (41:5)
Ione
Hijaabu kupitia Qur - ani:-
"BASI
AKASEMA ; NAVIPENDA VITU VIZURI KWA KUMKUMBUKA MOLA WANGU. KISHA
(mafarasi) WAKAFICHIKANA NYUMA YA KIZIUIZI (Hijaabu, kwa kutiwa
zizini mwao)" (38:32)
Ijue
Hijaabu kupitia Qur-ani-
"NA
AKAWEKA PAZIA (Hijaabu) KUJIJINGA NAO??.." 19:170.
Ielewe
Hijaabu kupitia Qur-ani- "NA UNAPOSOMA QUR-ANI (inakuwa kama kwamba)
TUMETIA BAINA YAKO NA BAINA YA WALE WASIOAMINI AKHERA PAZIA LILILOFUNIKWA
(sana hata hawafahamu kinachosemwa)" (17:45)
Hizi
ndizo baadhi ya aya za Qur-ani Tukufu ambazo ndani yake limetajwa na
kutumika neno "Hijaabu". Kupitia aya hizi tunaweza kusema kuwa
Hijaabu ya Kiislamu ni:-
a)Sitara
ya kutokuchangayika pamoja wanume na wanawake.
b)Sitara
ya kutokusikia sauti ya mwanamke kwa mwanamume.
c)
Sitara ya mwili (mavazi) yaani kutoonekana mwili wa mwanamke ila na
maharimu zake tu.
Hii
ndio eleweko la Hijaabu kwa mtazamo wa kiislamu, kama
tutakavyolithibitisha hilo na kulijengea hoja kupitia Qur-ani yenyewe.
Hijaabu hailengi ila kuwa ni chombo cha kujenga na kuratibisha uhusiano
mwema uliopo baina ya jinsia mbili zihitajianazo na kutegemeana, mwanamume
na mwanamke. Huu ni utaratibu na nidhamu ya lazima inayozisaidia jinsia
mbili hizi kuistawisha dunia na kuyafurahia maisha katika misingi
waliyowekewa na Mola Muumba wao. Kila mmoja, mwanamume na mwanamke
ameamrishwa na kukalifishwa kuishi kwa kuufuata utaratibu na nidhamu hii.
Hii ni kwa ajili ya kuidhibiti na kuitawala nguvu ya kimaumbile iliyopo
baina ya jinsia mbili hizi. Nguvu ambayo ina athari kubwa katika kuvuruga
na kuharibu mwenendo na silka
nzima ya mwanadamu. Mvuto na matamanio ya kijinsia alio nayo mwanamume,
yanapatikana pia kwa mwanamke. Kila mmoja kwa mwenzie ni mfano wa sumaku
inayokivuta chuma na hatimaye kukinasa na kushikamana nacho. Haya ndio
maumbile yaliyokamilika na chanzo/sababu yake ya msingi ni "Homonsi"
alizoumbiwa kila mmoja wao. Ni kwa kulijua na kuzingatia tabia hii ya
maumbile ya mwanadamu ndio tunaikuta Hijaabu hata katika vilabu vya
Mwenyezi Mungu Mtukufu vilivyoitangulia Qur-ani.
Hijaabu
ya Kiislamu haikomelei tu katika kusitiri na kuhifadhi mapambo (sehemu
zenye kuamsha na kuchochea fitna kati ya mwanamume na mwanamke), na
kuinamisha macho tu bali Hijaabu ni pamoja na:-
1·Kutokukaa
faraghani mwanamume na mwanamke. Haya ndiyo maelekezo na mafundisho ya
Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie - kupitia kauli yake:-"Asikae,
asikae, rafaghani mmoja wenu na mwanamke ila (awe pamoja na mwanamke huyo)
maharimu (yake, baba, kaka, babu n.k). Bukhariy na Muslim.
2·Kutogusana
mwili na mwanamume na mwanamke. Haya ndio mafundisho ya Uislamu kupitia
kauli ya Mtume wa Uislamu- Rehema na Amani zimshukie:- "Mmoja wenu
kuchomwa kichwani kwake na sindano ya chuma na bora kwake kuliko kumgusa
mwanamke asiye halali yake" Twabaraany. Amesema mkewe Bwana Mtume ,
Bi Aysha- Allah amuwiye radhi: "Wallah! Mkono wa Mtume wa Mwenyezi
Mungu Haukupata kabisa kumgusa mwanamke (asiye halali yake), ila alikuwa
akipeana nao ahadi kwa maneno (kwa kuzungumza) tu"
3·Mwanamke
kutokulegeza sauti yake mbele ya mwanamume. Tusome: ENYI WAKE WA MTUME,
NINYI SI KAMA YOYOTE TU KATIKA WANAWAKE WENGINE (ninyi wakeze Mtume). KAMA
MNATAKA (kufanya jambo la) KUMCHA ALLAH, BASI MSILEGEZE SAUTI (zenu
mnaposema na wanaume) ILI ASITAMANI MTU MWENYE UGONJWA MOYONI MWAKE (kufanya
mabaya na nyie) NA SEMENI MANENO MAZURI " (33:32). Semezo (kihitwaabu)
la aya hii linaelekezwa moja kwa moja kwa wakeze Bwana Mtume lakini amri
hii inawahusu na kuwaenea wanawake wote wa Kiislamu.
4·Kuzuia
picha, magazeti, majarida, vipeperushi, nakala na matangazo ambayo kwa
namna moja au nyingine huchochea na kuamsha tmaa na matamanio ya kimwili.
5·Mwanamke
kujitia manukato na kupita mbele ya wanaume . Bwana Mtume - Rehema na
Amani zimshukie - anatahadharisha juu ya hili kwa kutuambia "Mwanamke
yeyote atakayejitia manukato na kupita mbele ya wanamume ili waipate
harufu ya (manukato) yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu (anapata dhambi
za kuzini kwa sababu ya kushawishi kwake zinaa) na kila jicho (limtazamalo)
pia ni zinifu" Abuu Daawoud, Tirmidhiy, Nasaai, Ibn Khuzaymah na Ibn
Hibban.
Haya
ni baadhi tu ya maeneo yanayoguswa moja kwa moja na Hijaabu ya Kiislamu.
Msingi na asili ya suala la Hijaabu ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu ndani ya Qur-ani Tukufu isemayo "NA WAAMBIE WAISLAMU WANAWAKE
WAINAMISHE MACHO YAO, NA WAZILINDE TUPU ZAO WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO
VYAO ISIPOKUWA VINAVYODHIHIRIKA (nao ni uso na vitanga vya mikono). NA
WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO, NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA
KWA WAUME ZAO, AU BABA ZAO, AU BABA ZA WAUME ZAO (wakwe zao) AU WATOTO WAO,
AU WATOTO WA WAUME ZAO, AU KAKA ZAO, AU WANA WA KAKA ZAO, AU WANA WA DADA
ZAO, AU WANAWAKE WENZIWAO, AU WALE ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KIUME (watumwa
wao) AU WAFUASI WANAUME WASIO NA MATAMANIO ( kwa wanawake) AU WATOTO AMBAO
HAWAJAJUA MAMBO YANAYOHUSU UKE, WALA WASIPIGE MIGUU YAO ILA YAJULIKANE
WANAYOYAFISHIA KATIKA MAPAMBO YAO NA TUBIENI NYOTE KWA ALLAH ENYI WAISLAMU
ILI MPATA KUFAULU" (24:31).
Alisema
Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - wakati Asmaa Bint Abuu Bakri -
Allah awawiye radhi wote - alipoingia kwa Mtume akiwa amevaa nguo nyepesi:
"Ewe Asmaa, hakika mwanamke anapofikilia umri wa kupata hedhi (anapovunja
ungo) haifai kuonekanwa (mwili) wake ila hiki na hiki. Na (Mtume)
akaashiria uso na vitanga vyake" Abuu Daawoud.
Miongoni
mwa sharti za Hijaabu ya vazi la mwanamke wa Kiislamu ni kwamba:-
a)Isiwe
nguo yenyewe ni pambo linaloweza kumvutia mtazamaji. Hilo ndilo eleweko na
fahamisho la kauli ya Allah isemayo" "WALA WASIDHIHIRISHE
MAPAMBO YAO??." (24:31) Na kauli isemayo, "NA KAENI MAJUMBANI
MWENU, WALA MSIONYESHE MAPAMBO YENU KAMA WALIVYOKUWA WAKIONYESHA MAPAMBO
YAO WANAWAKE WA ZAMA ZA UJAHILI (Ujinga ukafri)??.' (33:33).
b)Iwe
nzito isiwe nyepesi ionyeshayo rangi ya mwili. Hii ni kutokana na
kauli ya Mtume isemayo:" Watakuwepo mwisho wa umati wangu wanawake
watakaovaa (lakini) wako uchi. Vichwani mwao kuna nundu (kutokana na
mitindo ya nywele) kama nundu za
ngamia. Walaanini kwa kuwa wao wamelaaniwa??" Ahmad.
c)Isiwe
yenye kubana sana kiasi cha kuonyesha ramani/finyango la mwili.
d)Isiwe
imetiwa manukato au kufukizwa kwa udi, Haya ni kwa mujibu wa kauli ya
Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie aliposema" Mwanamke yeyote
atakayejitia manukato, kisha akapita mbele ya wanaume ili waipate harufu
yake, basi yeye ni mzinifu",
e)Isifanane
na nguo za wanaume, hivyo ndivyo tunavyofahamu kutokana na kauli ya Bwana
Mtume - Rehama na Amani zimshukie - isemayo: "Si katika sisi mwanamke
mwenye kujishabihisha na wanaume wala mwanaume mwenye kujishabihisha na
wanawake. Twabaraaniy na Ahmad.
|