|
Hijabu ambayo Uislamu
umeifaradhisha na kumuwajibisha mwanamke, hamtakii mwanamke huyu ila
kulinda na kuchunga heshima yake na utu wake kupitia uvaaji, sauti na
kuchanganyika kwake na jinsia ya kiume ili asibughudhiwe na jinsia hiyo
na asiwe yeye ndio
kichocheo cha fitina na fisadi katika jamii.
Kwa mantiki hii tunaruhusika
kusema
kwa kinywa kipana kabisa kwamba hijabu ya Kiislamu ni HIFADHI
na HIMAYA kwa wanawake na wala sio KIFUNGO AU KIPINGAMIZI cha
kusitisha na kuzuia harakati za mwanamke katika kuchangia maendeleo yake
binafsi na yale ya jamii kwa ujumla.
Kama ambavyo Hijabu isivyomzuia mwanamke kufanya shughuli za ndani
ya
nyumba yake ndivyo hivyo hivyo haimzuii kufanya kazi nje ya nyumba
yake ingawa kubakia nyumbani ni bora zaidi kwake kuliko huko kutoka,
kutoka kwake nje ya nyumba yake ni pale atakapokuwa na haja ya kufanya
kazi ili kujikimu kimaisha au kazi hiyo inamuhitajia
yeye kwa maana kuwa hakuna afaaye kwa kazi hiyo ila ni yeye tu.
Ni katika mazingira haya na yenye ndio mwanamke wa Kiislamu mwenye
kumuamini ALLAH na siku ya mwisho anaweza kutoka nje ya nyumba yake.
Sheria inaliweka na kulirejesha suala hili katika maafikiano na
mapatano baina ya mke na mumewe au binti na walii wake lakini chini
ya msingi ya sheria na sio chini ya matashi na matakwa yao.
Hali kadhalika linarejea kushabihiana nayo katika wajibu na
majukumu ya kila mmoja wao yaani mke
na mume katika nyumba na maisha kwa ujumla.
Ama
suala la kufanya kazi kisheria ni haki na wajibu wa
kila mtu bila ya kujali jinsia yake muda wa kuwa kazi/shughuli
hiyo:-
-
Anaiweza
na kuimudu
-
Inalingana
na maumbile yake ya asili
-
Inampa
maslahi sambasamba na kuchunga utu na heshima yake.
-
Haina
madhara kwake wala kwa jamii
Mwenyezi
Mungu Mtukufu anatuambia kuhusiana na amali njema na kazi ikiwa ni
miongoni mwa hizo amali njema, tusome na tujifunze: “WAFANYAJI MEMA,
WANAUME AU WANAWAKE HALI YA KUWA NI WAISLAMU, TUTAWAHUISHA MAISHA MEMO, NA
TUTAWAPA UJIRA WAO (Akhera)
Mkubwa
(16:97).
Tujifunze
kupitia aya hii:-
-
Usawa
wa Mwanamume na mwanamke katika kutenda amali
njema (pamoja na kazi)
-
Kufanya
kazi ni katika jumla ya matendo ya dini kama mfumo sahihi na maisha .
-
Kufanya
kazi katika misingi na mazingira ya Kiislamu.
-
Kazi
ni sababu (wasila) ya kupatia maisha mema leo duniani na kesho akhera.
Tuendelee
kuogelea katika bahari ya kazi ndani ya Qur-ani Tukufu “MOLA WAO
AKAWAKUBALIA”
( Maombi yao kwa kusema )
“HAKIKA MIMI SITAPOTEZA JUHUDI” (Amali) YA MFANYA JUHUDI
MIONGONI MWENU, MWANAUME AU MWANAMKE, NYINYI
KWA NYINYI
Tumefahamu
kupitia aya hii:-
Kauli jumla ni kuwa hakuna aya
ndani ya Qur-ani
Tukufu
au hadithi katika sunnah ya Mtume – rehema na Amani zimshukie –
inyomnyima mwanamke haki yake ya kusoma na kufanya kazi.
Huu ndio ukweli na Historia inaukiri na kuukubali.
Hebu tuzipekue kwa pamoja kurasa za historia ziturejeshe katika
zama za Bwana Mtume.
Tuione nafasi ya mwanamke na mchango wake katika jamii ile.
Kumbukumbu sahihi za kihistoria zinamuonyesha mwanamke wa Kiislamu
zama za Mtume akibeba majukumu na kushiriki katika shughuli mbalimbali
za kijamii. Tunamkuta
mwanamke hata katika midani
ya vita kama
muuguzi akiwatibu majeruhi wa vita na yote
hii ni katika kutekeleza Uislamu kivitendo.
Lakini
pamoja na ruhusa hii ya kutoka nje na
kufanya kazi aliyopewa mwanamke na Uislamu
bado hatuwezi kuukana
ukweli unaosisitizwa na Uislamu kuwa nafasi ya mwanamke
ndani ya nyumba yake ni bora zaidi kuliko
nafasi yake ya nje
nyumba.Ukweli huu unadhihishwa na kujitokeza kupitia kauli ya Bwana
Mtume Rehema na Amani zimshukie: Wanawake ni vivutio, na hakika
Mwanamke
hutoka nyumbani mwake bila ya kukusudia
ubaya
wowote. Basi Shetani humchomozea
na kumatangulia na kumwambia : Hakika
wewe humpitii yeyote ila atapendezwa
nawe. Na hakika mwanamke
atavaa nguo
zake kisha aulizwe : Unakwenda wapi?
Aseme ( Ajibu ) Nakwenda
kumtazama mgonjwa, au nakwenda mazikoni, au nakwenda kuswali.
Mwanamke
hakumwabudu
Mola
wake
kama anavyoabudu nyumbani mwake". Twabaraany.
Utokaji
wa mwanamke nje ya nyumba yake
unaweza kuwa ni wajibu
kwa maana ya
wajibu. Vipi , maana inawezekana
kabisa Mwanamke
akawa hana mtu wa kumkimu kimaisha baada ya kufiwa na mumewe au
Baba yake na pengine
ana watoto na wazazi wanaomtegemea. Hapa katika mazingira haya na
yenye kushabihiana
nayo lazima bali ni wajibu kwake
atoke nje kufanya
kazi kwa ajili ya kujimu yeye mwenyewe a wanaomtegemea .
Imethibiti
katika riwaya iliyopokelewa na
Imani Bukhaariy -Allah amrehemu kutoka
kwa Biaysha
amuwiye radhi – kwamba Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie –
aliwaruhusu /aliwapa idhini wakeze kutoka nje kwa ajili ya kudhi
haja zao ( mahitaji) mbali mbali. Kadhalika ni wajibu mwanamke
atoke nje kwenda kutafuata elimu ambayo
haipatikani ndani ya nyumba yake , hii ni kutokana na ukweli kuwa
kutafuta elimu
ni faradhi ya lazima mno katika Uislamu.
Zama
za Bwana Mtume wanawake walikuwa
wakitoka kwenda kumuuliza Mtume, mambo
mbali mbali yahusianayo na dini
kutokana
na kiu na pupa yao ya kutaka kuijua dini yao waliomba wapewe siku
yao maalum ili waweze kumuuliza Mtume
mambo ya ndani yanayomhusu wanawake ambayo ni aibu kuyasema mbele
ya wanaume. Hii ndio sababu Bwana Mtume aliwakataza
waume kutowazuia wake zao kwenda Msikitini watakapowaomba ruhusa .
Kwa
sababu kwenda kwao Msikitini hakukuwa ni kwa
ajili ya swala tu, kwani kama ni hivyo basi
kuswali kwao majumbani mwao ni bora na
na kuna thawabu zaidi kuliko Msikitini. Lakini
kwenda kwao Msikitini kulikuwa ni kwa
ajili ya kujifunza dini, kusikiliza wahyi (ufunuo)
uliomshukia Mtume na kujifunza
swala Kivitendo nyuma ya mwenyewe Bwana Mtume .
Tumtegee sikio Bwana Mtume Rehema
na Amani zimshukie –akituambia watakapo kuombeni wake zenu ruhusa
ya kwenda
Msikitini basi waruhusuni Muslim.
Hii ni kwa sababu ya Msikiti wakati wa
Mtume ulikuwa unamaanisha kila kitu ulikuwa ndio kituo cha kijamii
Msikitini
ulikuwa ni:
-
Nyumba
ya Ibada
-
Kituo
cha elimu ( Shule
-
Idhaa
ya Jamii ( Redio) Jengo la mawasiliano
-
Mahakama
-
Khazina
ya Jamii
-
Makazi
ya masikini na wasiojiweza
-
Bunge
la Waisilamu
-
Mahala
pa kuliandalia jeshi
na
…………………….na …………………….
Hali
kadhalika ni wajibu kwa mwanamke kutoka kwenda kufanya kazi ambayo yeye
ana ujuzi nayo na hakuna mtu mwingine anayeweza kuifanya vizuri zaidi ila
ni yeye tu na kama hakwenda jamii itaathirika kwa kukosa huduma hiyo.
Kama ambavyo pia ni wajibu atoke kwenda kushiriki katika mambo
mbalimbali ya kheri, kutoa msaada wa dharura katika majanga mbalimbali.
Pias mwanamke anaweza kumsaidia mumewe katika shghuli za kutafuta
maisha kama inavyokuja katika riwaya ya Bi Asmaa Bint Abu Bakri – Allah
awawiye radhi, kwamba Bi. Asmaa alimwambia baba yake; Unanioza Zuberi na
il-hali yeye hana mali yoyote, hana mtumwa na wala hana chochote zaidi ya
farasi na ngamia wake .
Asmaa anaendelea kusimuliwa (basi baada ya kuolewa) nilikuwa
nikimtafutia na kumpa chakula farasi wake huyo na kumpondea na kumlisha
tende ngamia wake (pia) na nilikuwa nikichota maji na kutengeneza vifaa
vya kutunzia maji. (Pia) nilikuwa nakoboa nafaka na kubeba tende kichwani
kutoka shambani.
Mpaka
Abubakri (baba yangu akanionea huruma) na kuniletea mfanyakazi
akanisaidia kushughulikia farasi basi ikawa kama vile
amenikomboa.
Siku moja nilikutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani
zimshukie akiwa na maswahaba wake, nami nikiwa nimejitwika tende
kichwani akasema Ikh, ikh, ili amketishe ngamia wake na kunibeba nyuma
yake.
Nikaona haya kwenda pamoja na wanamume (nikashindwa kupanda)
nikamkumbuka Zuberi (mume wangu) na wivu wake kwani alikuwa na wivu
kupindukia.
Bwana mtume akatambua kwamba mimi naona haya (akaenda zake)
Nikafika kwa Zuberi na kumuhadithia yaliyotokea, akaniambia
“WALLAH
Mzigo uliokuwa nao kichwani ulikuwa ni jambo zito zaidi kuliko huko
kupanda kwako (ngamia) wake (Mtume) akimaanishia ungepanda tu –
Bukhaariy na Muslum.
Tunachojifunza
katika hadithi hii ni kwamba:-
Pamoja
na kufanya kwake kazi nje ya nyumba yake bado maswahaba walikuwa
wakilichukia jambo hili kwa hoja kuwa linashusha hadhi ya mume machoni mwa
jamii.
Kwa kuwa
hili halimaanishi zaidi kuwa yeye kashindwa kumkimu mkewe kwenye
kufanya kazi, maadam
kuna haja ya kufanya hivyo.
Hii ni kutokana na ushahidi wa Mtume kumwona Bi. Asmaa akifanya
kazi na asimkemee au kumkataza, kwa hivyo ni dhahiri kuwa Mtume alilikiri
hilo.
Historia ya Uislamu imesheheni mifano mingi inayoonyesha kujuzu
kufanya kazi kwa mwanamke, tuisome na tutaona.
MADA
INAENDELA :
INSHAALLAH !
|